Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa bleacherreport.com
iliwahi kutoa ripoti ya wachezaji kadhaa ambao hupaswi kuwaamini kwa
mpenzi wako. Hadi kufikia mwezi October mwaka 2011 hawa ndio wachezaji
waliyokuwa wanatajwa kuwa, hutakiwi kuwapa nafasi ya kuwa karibu na
mpenzi wako.
- John Terry aliwahi kuingia katika headlines ya kutembea na mke wa mchezaji mwenzake na rafiki yake wa zamani wa Chelsea. Terry alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa Wayne Bridge ambaye ni beki wa zamani wa klabu ya Man City. Kitu ambacho kilileta uadui mkubwa kiasi kwamba Wayne Bridge ilimbidi astaafu kucheza timu ya taifa ya Uingereza inadaiwa ili asikutane na Terry.
- David Beckham huyu anatajwa kuwa ni handsome sana kitu ambacho kimepelekea kuwa anapata mikataba mingi ya biashara kutokana na muonekano wake, hivyo hupaswi pia kumuweka karibu na girlfriend wako licha ya kuwa hana kashfa nzito kama ilivyo kwa John Terry.
- Ryan Giggs huyu anaonekana ni mtu mwenye busara lakini amewahi kuingia katika kashfa nzito ya kutoka kimapenzi na mke wa ndugu yake wa damu Rhodri kitu kilichopelekea kutoelewana na ndugu yake kwani alikuwa katika mahusiano na shemeji yake Natasha kwa miaka 8, hivyo Rhodri aliamini kuwa Giggs alidhamiria kufanya hivyo.
- Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney aliwahi kuingia katika kashfa ya kutoka kimapenzi na Jennifer Thompson msichana ambaye anajiuza na maarufu sana kwa wateja wake kama Juicy Jeni, mrembo huyo ndiye aliyevujisha taarifa za kutoka kimapenzi na Rooney wakati mkewe Coolen alikuwa na ujauzito wa Kai.
- Thierry Henry huyu mahusiano yake na Claire Merry yalivunjika kutokana na kukosa uaminifu kwa mpenzi wake baada ya magazeti ya Kiingereza kuripoti kuwa alikuwa akichepuka na make-up artist Sadie Hewlett ila siku kadhaa mbele mpenzi wake Claire alifumania meseji katika simu ya Henry.
0 maoni:
Chapisha Maoni