1.0. UTEUZI KIDATO CHA 5 – AWAMU YA PILI 2015. Ufaulu wa watahiniwa Kidato cha Nne kwa mwaka 2014 kuanzia daraja la Distinction hadi Credit yaani GPA ya 5.0 hadi 1.6 ni watahiniwa 73,754 wakiwemo wasichana 27,680 na wavulana 46,074 sawa na asilimia 37.48 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 ni jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wavulana 31,700 na wasichana 23,303. Aidha, wanafunzi waliochaguliwa na kujiunga na vyuo vya Ufundi ni 479 wakiwemo wavulana 332 na wasichana 147. Matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2015 yalitangazwa tarehe 30/6/2015. Wanafunzi wote walitakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 18/7/2015. Tarehe ya mwisho ya kuripoti ilikuwa ni tarehe 31/7/2015. Hata hivyo kulitokea maombi mengi ya kubadili shule/ tahasusi. Maombi hayo yalishughulikiwa kwa kuzingatia kutojaza baadhi ya shule na nyingine kuwa wazi. Baada ya mabadiliko haya bado kulikuwa na maombi mengine ambayo yalihusu kubadili shule/tahasusi ndani ya Mkoa au Halmashauri. OWM- TAMISEMI iliwaandikia barua Makatibu Tawala wa Mikoa kushughulikia maombi yaliyoko ndani ya mikoa yao. 2.0 .HALI ILIVYO HADI SASA. Hadi sasa jumla ya wanafunzi 8,945 wameshapatiwa fursa ya masomo ambapo jumla ya wanafunzi 8,822 wamepangiwa kusomea ualimu UDOM. Kati yao wanafunzi 7,042 watasoma SCIENCE, MATHEMATICS AND ICT(Dip, Ed SMICT) na wanafunzi 1,780 watasoma Ordinary Diploma in Primary Teacher Education (ODPE). Aidha jumla ya wanafunzi 123 wamechaguliwa kujiunga na shule mpya ya serikali ya St. Peter’s Liuli iliyopo Halmashauri ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma iliyopata usajili Julai 2015. Wanafunzi hawa ni wa tahasusi za HGL na HKL. Bado wanafunzi 9,806 hawajapata fursa ya kuchaguliwa. OWM TAMISEMI imewaandikia barua Makatibu Tawala wa mikoa ya kuwataka kuwasilisha idadi ya wanafunzi ambao hawajaripoti kwenye shule zilizoko kwenye mikoa yao kwa kila tahasusi. Tayari baadhi ya mikoa imeanza kuwasilisha taarifa za wanafunzi wasioripoti. Baada ya kupokea taarifa hizi kutoka mikoa yote, second selection kwa wanafunzi waliobakia itafanyika tarehe 30/8/2015 - 2/9/2015. Watakaochaguliwa watatangazwa pamoja na tarehe ya kuripoti shuleni. Utaratibu utawekwa wa kufidia siku ambazo hawakusoma kwa kutumia siku za mapumziko mafupi (mid term) na muda mwingine muafaka.
KUHUSU SECOND SELECTION KIDATO CHA TANO

Blog inayotoa habari kila siku
Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa
0 maoni:
Chapisha Maoni