Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » MBUNGE AIKACHA CHADEMA, ARUDI KANISANI

MBUNGE AIKACHA CHADEMA, ARUDI KANISANI

 
MBUNGE wa Karatu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Israel Natse, hatimaye amejitoa rasmi katika siasa na kurudia kazi yake ya Uchungaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Natse alisema makubaliano yake na chama, walimwomba agombee kipindi kimoja tu na sasa anapisha mwingine. “Narudi kwenye kazi yangu ya Uchungaji, sasa naachana na siasa. Huu ndio wito wangu nilioitiwa na Mungu wa uchungaji,” alisema.

Badala yake, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alithibitisha kuwa makada wake watano, wamejitosa kutaka kumrithi Mchungaji Natse. Alitaja kuwa ni Lazaro Masai, Francisca Duwe, William Kumbalo, Kwamala Aloyce na Pascal Gutt.

Aidha, alisema katika Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amejitokeza kutetea ubunge wake, lakini akikabiliwa na upinzani kutoka kwa Nsajigwa Mwakatobe na Noel Olevaroya.

Katika jimbo la Arumeru Mashariki, hakuna mwana Chadema aliyejitokeza kumpinga Joshua Nassari. Alisema katika Jimbo la Longido wamejitokeza Francis Oleikayo na Paulina Lucas, anayegombea kupitia Viti Maalumu.

Katika Jimbo la Monduli wagombea ni Cecilia Pareso, Patrick ole Mongi, Navaya Ndaskoi, Julius Kalanga na Japhet Silonga.

Waliojitokeza katika Jimbo la Ngorongoro ni Daudi ole Mtala, Samwel ole Ndimama na katika Jimbo la Arumeru Magharibi ni Benjamini Laizer, Gibson Mesiyek, Mchungaji Philemon Langai Mollel na Samwel Sirikwa. Lazaro alisema mchakato wa kura za maoni, utafanyika kesho katika majimbo yote.

Kwa upande wa chama tawala, CCM mkoani Arusha, Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Alphonce Kinamhala aliwataja waliojitosa kuwania Jimbo la Arusha Mjini wakilenga kumng’oa Lema ni 14.

Hao ni Philemon Mollel `Monaban’, Swalehe Kiluvia, Victor Njau, Justin Nyari, Mustafa Panju, Thomas Munisi, Hamis Shaaban, Wakili Edmund Ngemera, Dk Moses Mwizarubi, Andrew Lyimo, Lukija Malugo, Mohammed Omari na Emmanuel ole Nyoro.

Jimbo la Monduli lililoachwa rasmi na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa limevutia wagombea sita, akiwemo Namelok Sokoine, Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mtoto wa Waziri Mkuu mwingine wa zamani kutoka Monduli, Edward Moringe Sokoine.

Wengine ni Sakaya Kabuti, Rolinyu Mkoosi, Lotha Sanare, Fayani Tayai na Amani Torongei. Katika Jimbo la Ngorongoro, mbali ya Mbunge anayemaliza muda wake, Saning’o ole Telele, yumo pia Dk Eliaman Loltaika, Elias Longari, Joseph Parasambei, Patrick Kasongo na Wiliam ole Nasha. Kwa upande wa Jimbo la Karatu, wapo John Dodo, Dk Wilibard Lory, Joshua Mbwambo na Rajabu Malewa.

Arumeru Mashariki ni Elirehema Kaaya, Jackson Mahoho, John Sakaya, Angela Pallangyo, William Sarakikya, Dk Daniel Palangyo na Sioi Sumari ambaye mwaka 2012 aliwania ubunge katika jimbo hilo wakati wa uchaguzi mdogo, uliotokana na kifo cha aliyekuwa mbunge na baba mzazi wa Sioi, Jeremiah Sumari. Katika Uchaguzi huo, Joshua Nassari wa Chadema alitwaa ushindi.
Chanzo: Habari leo
Blog inayotoa habari kila siku Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. JAFAR NZOWA JR - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger