Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Manispaa ya Bukoba, Chifu
Karumuna amebwaga manyanga na kujiunga na Chadema.Akizungumza
baada ya kukabidhiwa kadi mpya ya Chadema juzi, mwenyekiti huyo wa
zamani wa UVCCM, ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Kahororo alisema
hakutendewa haki na chama chake, alichokituhumu kumpora ushindi pamoja
na kuongoza katika kura za maoni kutetea wadhifa wake.Jina la Karumuna
liliondolewa kwa madai kuwa hakuwa na sifa za kugombea udiwani, uamuzi
alioupinga na kuamua kuhamia Chadema.Karumuna anadaiwa kuondoka na
wanachama wengine zaidi ya 100 kutoka CCM.Mwenyekiti
wa Chadema Manispaa ya Bukoba, Victor Sherejei alisema Karumuna
amechukua uamuzi wa busara, kwani hata kabla ya kuhama CCM alikuwa
mstari wa mbele kutetea haki za wananchi.
Kilindu alisema wameamua kujiuzulu nafasi hizo kwa kuhofia usalama wa maisha yao na familia zao.
Alisema kujiuzulu kwao kunatokana na kuvuja kwa siri za ndani za mchakato wa kura za maoni, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Mwenyekiti
huyo alimtuhumu mmoja wa wagombea kwenye kura za maoni kutuma kundi la
vijana kwa ajili kumdhuru, huku pia akitishiwa kuchomewa moto nyumba
yake na ofisi ya CCM. Alisema pamoja na kwamba hakutoa taarifa za
vitisho hivyo polisi, lakini uamuzi wa kujiuzulu ndiyo njia pekee ya
kuokoa maisha yake.Alisema kujiuzulu kwao kunatokana na kuvuja kwa siri za ndani za mchakato wa kura za maoni, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
0 maoni:
Chapisha Maoni