Licha Tundu Lissu kusisitiza kuwa Mwenyekiti wake yuko vizuri, Mwenyekiti huyo amezungumza na Waandishi wa Habari leo ambapo amesema afya yake imeimarika na anendelea vizuri.
Aidha, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana aliugua ghafla akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa baada ya kuchukua fomu za kugombea urais katika Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC).
Katika msafara huo wakiwa njiani Mbowe na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walikuwa wamechomoza kwenye gari wakiwapungia wananchi waliojitokeza kwenye maandamano hayo lakini baadae hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni