Jeshi la polisi kanda maalumu ya DSM lakanusha kupiga marufuku maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea urais chadema.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya DSM Suleiman Kova amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yanayo anzia CHADEMA kwenda NEC,lakini ya kutoka Nec kwenda makao makuu ya CUF buguruni hawayatambui.-ITV Tanzania
Wakati kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kamishna Suleiman Kova akitoa taarifa za Polisi kuzuia maandamano ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambayo yalielezwa kuanzia bunguruni ofisi za CUF badala ya Kinondoni makao makuu ya CHADEMA kwaajili ya kumsindikiza mgombea wao kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais ukawa kupitia mwenyekiti mwenza wake ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameeleza kuwa hawajapata taarifa za zuio hilo kuanzia ofisi za CUF badala yake wataendelea na ratiba yao kama ilivyo pangwa.-ITV Tanzania
0 maoni:
Chapisha Maoni