Hayo yamesemwa muda mfupi Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika Kikao cha Dharula cha Baaraza la kuu la uongozi wa chama hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa Lipumba .
Amesema katokana na Kanuni za CUF wamekubaliana kwa pamoja kuunda kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi sita na baadae kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.
Ameongeza kuwa Kamati hiyo itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif na mwenyekiti wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na kushirikiana na Vyama vyengine vinavyounda UKAWA ambapo anadai itakuwa na jukumu lingine la kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.
0 maoni:
Chapisha Maoni