Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » SHERIA MPYA LIGI KUU YA UINGEREZA

SHERIA MPYA LIGI KUU YA UINGEREZA

epl-logo

BAADHI YA SHERIA MPYA ZITAKAZOTUMIKA LIGI KUU UINGEREZA 2015/16


Msimu mpya wa ligi kuu Uingereza unakaribia kuanza mnamo mwisho wa wiki, wachezaji na viongozi wa vilabu hawana budi kufata sheria mpya za ligi kuu.
Mabadliko makubwa yaliyofanywa katika sheira hizo za ligi kuuUingereza ni kuhusu wachezaji kumzonga refarii, wachezaji watakao danganya wameumizwa, vile makocha na viongozi watapata adhabu kwa matendo mbali mbali watakayo onyesha.
KUDANGANYA UMEUMIA ILI MPINZANI APEWE KADI NYEKUNDU AU YA NJANO.
Mchezaji atakayedanganya ameumizwa atapewa adhabu.
Sheria hii iko hivi
  • Mchezaji A ametolewa nje kwa kitendo cha kumchezea rafu mchezaji B.
  • Kadi hii nyekundu inaweza kufutwa baada ya refa kuangalia tena tukio hilo na kama akigundua kuwa mchezaji B alidanganya kuwa ameumizwa basi kadi hiyo na adhabu itafutwa.
  • Na mchezaji B ambaye alidanganya kuumizwa atakabiliwa na adhabu ya kutocheza mechi 3.
Andy-Carroll-red-card
Mfano katika mchezo wa West Ham dhidi ya Swansea mnamo mwezi wa Februari 2014, mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll alimchezea rafu mchezaji wa Swansea Flores na kupelekea Andy Carroll kupewa kadi nyekundu. Lakini ilipokuja kuangaliwa tena ilionesha kuwa Flores alidanganya kama ameumizwa na rafu ile kitu ambacho kwa sheria hii mpya tungeshuhudia kufutwa kwa kadi nyekundu ya Andy Carroll na kupewa adhabu ya kutocheza mechi tatu kwa mchezaji wa Swansea Flores.
BENCHI LA UFUNDI NA ENEO LA MAKOCHA
  • Kocha akionesha ishara ya mchezaji apewe kadi, akipiga teke chupa za maji au akipiga makofi ya kebehi kwa maamuzi ya refa.
  • Kwanza atapewe onyo.
  • Hatua itakayo fata ni kutolewa katika eneo la ufundi na kupelekwa jukwaani
KUMZONGA REFARII/MWAMUZI WA KATI/WASAIDIZI WA MUAMUZI NA MAKAMISAA
villa
  • Wachezaji wawili na zaidi wakimfata refarii na kumzonga au wakiwafata wasaidizi wa refarii na makamisaa.
  • Kitendo hichi kitapelekea klabu kupewa adhabu kama kitendo hicho kitaripotiwa na refarii wa mchezo.
  • Awali ilikuwa wachezaji watatu na zaidi lakini sasa imepunguzwa.
SHERIA YA KUOTEA
Mchezaji atakuwa ameotea pale tu
  1. Mchezaji aliye eneo la kuotea amejaribu kuucheza mpira uliokaribu nae ambapo kitendo hicho kitapelekea kuathiri uchezaji wa mpinzani.
  2. Mchezaji aliye eneo la kuotea kama atafanya kitendo ambacho kitapelekea kuathiri mchezo wa mchezaji wa timu pinzani-(hapa si lazima auchezae mpira).
ROJO OFFSIDE
Mchezo kati ya Manchester United na Stoke mnamo mwezi wa Desemba 2, 2014 ambao uliishia kwa United kushinda kwa goli 2-1. Juan Mata alipiga mpira katika eneo la hatari la timu ya Stoke na beki Marcos Rojo wa Manchester United alijaribu kuucheza mpira huo akiwa katika eneo la kuotea lakini hakufanikiwa kuugusa, mpira huo ulitinga wavuni na Manchester United kupata bao.
ROJO
Hali ingekuwaje kwa sasa.
Kwa sheria hii ya sasa Manchester United wasingepata bao, kwani kitendo cha Marcos Rojo kujaribu kuucheza mpira ule kulipelekea athari katika mchezo wa mpinzani, hapa tunamzungia golikipa Asmir Begovic kwani kitendo cha Marcos Rojo kujitahidi kuucheza mpira ule kwa namna moja au nyingine kulimfanya golikipa huyo kupoteza mahesabu na mwisho wa siku Manchester United kupata bao.
ROJO 2
MPIRA MPYA
Mpira utakao tumika sasa ni Nike Ordem 3, utakuwa ndo mpira rasmi kwa ligi kuu Uingereza msimu wa 2015/16.
Kipi kipya katika mpira huu, watengenezaji wa mpira huu wanasema kuwa “Nike Ordem 3 unaonekana kiurahisi, unautulivu na haubadili uelekeo ovyo”
NIKE


Blog inayotoa habari kila siku Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. JAFAR NZOWA JR - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger