Nchini Italia kiungo ambaye amekuwa
gumzo kwenye soko la usajili akitajwa kuwa mbioni kujiunga na karibu
timu zote kubwa Paul Pogba amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo atakuwa
akiivaa kwa msimu ujao katika michuano mbalimbali ya ndani nan je .
Pogba mwenye umri wa miaka 22 anakabidhiwa jezi namba 10 baada ya mshambuliaji Carlos Tevez ambaye alikuwa anavaa jezi hiyo kuhamia Boca Juniors hali iliyofungua fursa ya jezi hiyo kukabidhiwa kwa Pogba.
Pogba anakuwa Mfaransa wa pili kuvaa jezi namba 10 kwenye klabu ya Juventus baada ya gwiji mwingine Michel Platini ambaye kwa sasa ni rais wa UEFA kuvaa jezi namba 10 katika miaka ya 80 wakati akiwa anaicheza klabu hii .
Ukiachilia mbali kuondoka kwa Tevez
kuacha jezi namba 10 kuwa wazi, wadadisi wa mambo wanaamini kuwa huenda
hii ikawa mbinu ya kumvutia mchezaji uyo kumfanya endelee kubaki na
Juventus hasa ukizingatia kuwa amepokea ofa nyingi zinazomtaka kuihama
klabu hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni