Baada ya
kujiunga na PSG kwa dau la paundi milioni 44, winga wa kimataifa wa Argentina,
Angel di Maria amewaandikia barua ya wazi mashabiki wa klabu ya Manchester
United ambayo ameichezea kwa mwaka mmoja.
Di Maria alisajiliwa na Man United
kutokea Real Madrid kwa ada ya paundi milioni 60 na kuvunja rekodi ya usajili
ya soka la England.
BARUA YA WAZI YA ANGEL DI MARIA KWA
MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED
"Naandika barua hii kuishukuru
familia nzima ya Manchester United kwa kuniunga mkono kwa mwaka mmoja niliokuwa
sehemu ya klabu.
Manchester United waliponichagua
kuwa sehemu ya timu yao, nilijisikia kuheshimiwa kwasababu nilijua klabu hii
ina maanisha nini na jinsi gani iliniamini.
Hata hivyo, nafahamu mambo
hayakwenda vizuri kama tulivyotarajia, naomba msamaha kwa hilo.
Katika maisha ya mcheza mpira, kuna
wakati mwingine mambo usiyotarajia na usiyoyataka yanatokea.
Nawahakikishia kwamba haikuwa
kujaribu. Nilijitahidi niwezavyo, lakini mpira sio kama hesabu: Mara zote kuna
vitu vingi vinavyoathiri vile unavyofikiria.
Samahani sana kwasababu sikufanya
kile nilichotarajia katika klabu hii kubwa na ya ajabu.
Natoa shukurani za pekee kwa bodi ya
wakurugenzi na utawala ya Manchester United, vilevile kila kiongozi na
wachezaji wenzangu walioniunga mkono.
Pia shukurani za pekee ziwaendee
mashabiki ambao mara zote waliniamini na kuonesha heshima na mapenzi makubwa.
Sasa ni wakati wa kujiunga na PSG,
lakini Utukufu wa Manchester United utabaki kwenye kumbukumbu zangu daima.
Nawatakia kila la kheri
Angel di Maria".
0 maoni:
Chapisha Maoni