WINGA
Godfrey Mwashiuya ametokea benchi na kuiadhibu timu yake ya zamani,
Kimondo kwa kuifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 jioni ya leo
Uwanja wa CCM Mbozi, Mbeya.
Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akabadilisha kikosi na timu ikapindua matokeo.
Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akabadilisha kikosi na timu ikapindua matokeo.
Beki Juma Abdul alimpisha Mbuyu Twite, kiungo Thabani Kamusoko akampisha Said Juma ‘Makapu’, winga Deus Kaseke akampisha Mwashiuya na mshambuliaji Malimi Busungu akampisha Amisi Tambwe.
Mwashiuya aliyesajiliwa Yanga SC msimu huu kutoka Kimondo, akafunga mabao mawili, Simon Msuva na Tambwe moja Yanga ikishangilia ushindi wa 4-1.
Yanga SC inaondoka Mbozi mara baada ya mchezo tu, kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya pia, kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Agosti 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Mudathir Khamis, Juma Abdul/Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Rajab Zahir, Thabani Kamusoko/Said Makapu, Simon Msuva, Salum Telela, Donald Ngoma, Malimi Busungu/Amisi Tambwe na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya.
0 maoni:
Chapisha Maoni