Ikiwa ndio kwanza ligi imeanza headline za EPL sio nani kamfunga nani tu, bali hata maisha ya mastaa wa EPL nayo pia yana-amake headline. Hivi sasa mchezaji wa West Ham Diafraa Sakho ana mashataka polisi kwa kosa la kushambulia mwanamke.
Kisa hiki kilitokea siku tatu kabla ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Arsenal ambapo walishinda kwa magoli 2 bila. Sakho alicheza karibia mechi yote dhidi ya Arsenal.
Diadra ambaye alinunuliwa kwa £3.5m mwaka jana alikamatwa kwenye nyumba yake huko Essex na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha East London. Makosa yake yameandikwa ni kusababishia majeraha na kumtolea lugha chafu mwanamke huyo.
Japokuwa taarifa hiyo ya polisi haikusema mwanamke huyo ni nani, ripoti za ndani zinasema atakua partner wake anaitwa Maya.
0 maoni:
Chapisha Maoni