Mabingwa wa kandanda Tanzania
bara, Young Africans wameinyuka Tanzania Prisons 2-0 katika mechi ya
kirafiki iliyopigwa uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Magoli ya Yanga yamefungwa na washambuliaji wake hatari, Malimi Busungu na Amissi Tambwe kwa kila kipindi.
Donald Ngoma na Geofrey Mwashiuya walijitahidi kucheza kwa kiwango kizuri, lakini walishindwa kucheka na nyavu.
Kiujumla Yanga imetandaza soka
murua katika mchezo huo uliokuwa wa kujipima nguvu kwa makocha wote
wawili, Salum Mayanga (Tanzania Prisons) na Hans van der Pluijm (Yanga).
Nao Prisons walijitahidi kushambulia mara kadhaa, lakini ngome ya Yanga ilikuwa imara.
Mbali na hayo, mechi hiyo ilitawaliwa na ubabe wa hapa na pale ambapo Mwinyi Hajji alitolewa kwa kadi nyekundu.
Mbali na hayo, mechi hiyo ilitawaliwa na ubabe wa hapa na pale ambapo Mwinyi Hajji alitolewa kwa kadi nyekundu.
Mwashiuya aliifungia Yanga
mabao mawili katika ushindi wa 4-1 waliovuna dhidi ya Kimondo FC katika
mechi ya kwanza ya kirafiki iliyopigwa mwishoni huko Vwawa Mbozi.
Mwishoni mwa Juma hili, Yanga inatarajia kushuka uwanjani tena kuchuana na Mbeya City katika uwanja huo wa Sokoine.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa shilingi 40,000/.
0 maoni:
Chapisha Maoni