Afisa habari wa klabu ya Simba
Hajji Manara jana alikuwa kivutio kikubwa kwenye siku ya Simba Day pale
alipoingia uwanja kuonesha kipaji chake cha soka wakati timu yake ya
viongozi wa Simba SC ilipokuwa ikicheza na wacheza filamu wa Tanzania
(Bongo Movies) mchezo uliokuwa wa utangulizi kabla ya mechi ya Simba SC
haijacheza na Sports Club Villa ya Uganda.
Manara
aliingia uwanjani akitokea benchi na mara baada ya kuanza kucheza mpira
mashabiki wa timu hiyo walianza kumshangilia Manara ambaye amekuwa na
maneno mengi tangu alipopewa wadhifa wa kuwa afisa habari wa klabu hiyo.
Hata
hivyo Manara hakucheza dakika zote zilizokuwa zimesalia kwani alitoka
na nafasi yake kuchukuliwa na kiongozi mwingine wa klabu hiyo.
Manara alisema mbali na kuwa msemaji wa Simba, yeye anakipaji cha kucheza mpira na amekuwa akicheza mpira tangu shule ya msingi.
Viongozi
wa klabu ya Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya
waigizaji wa Bongo movies goli lililowekwa kambani na kocha mkuu wa
Simba SC Dylan Kerr.
0 maoni:
Chapisha Maoni