UEFA
imetoa orodha ya wachezaji ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora wa
Ulaya kwa mwaka 2015. Majina ya wachezaji waliocheza fainali ya UEFA
Champions League kati ya Barcelona dhidi ya Juventus yametawala kwenye
orodha hiyo huku Lionel Messi na Paul Pogba wakipewa nafasi ya juu
kutwaa tuzo hiyo.
Winga wa Chelsea Eden Hazard pia
ameingia kwenye orodha hiyo akiwa ni mchezaji pekee kutoka kwenye ligi
ya England ambaye anapambana na wakali wengine kutoka La Liga na Serie
A. Tovuti rasmi ya UEFA imetoa taarifa zaidi juu ya listi hiyo
inayomjumuisha pia mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Ladha ya Barca-Juve imekuja bila
kipingamizi. Miamba ya Catalan iliyoshinda vikombe vitatu msimu uliopita
kwa kusaidiwa na washambuliaji watatu waliopewa jina la ‘utatu
mtakatiu’ unaoundwa na Messi, Luis Suarez pamoja na Neymar ambao wote
wapo kwenye orodha hiyo.
Wakati Juve wakitumaini kutwaa
taji lao la tatu msimu huu waliangukia pua mbele ya Barca lakini bado
Andrea Pirlo na Arturo Vidal wanaungana na Pogma kwenye orodha hiyo.
Wachezaji ambao walidhaniwa
wangeinia kwenye orodha hiyo lakini wamepigwa chini ni pamoja na
mshambuliaji wa Sevilla Carlos Bacca na winga wa Arsenal Alexis Sanchez.
Bacca aliifungia Sevilla magoli 28 pamoja na kuisaidia timu hiyo
kushinda taji la Europa League.
Wakati Sanchez yeye alifunga
magoli 25 na kuisaidia Arsenal kutwaa taji la FA lakini kuenguliwa kwao
kwenye orodha hiyo kumezua maswali mengi.
Watu wameanza kutabiri kuwa,
mshindi wa tuzo hiyo atakuwa ni miongoni mwa wachezaji waliocheza
fainali ya Champions League msimu uliopita huku Messi akipewa nafasi
kubwa pamoja washambuliaji wenzie kutoka Barcelona.
Agosti 12 watatangazwa wachezaji walioingia tatu bora wakari msindi atatangazwa Agosti 28 Monaco, Ufaransa.
0 maoni:
Chapisha Maoni