KLABU
ya Manchester United iko tayari kumuuza Victor Valdes baada ya Louis
van Gaal kukerwa na kitendo cha kipa huyo kugoma kuchezea kikosi cha
pili msimu uliopita.
Mlinda
mlango huyo mwenye umri wa miaka 33 ameachwa kwenye msafara wa United
uliokwenda ziara ya Marekani na anaendelea kufanya programu maalumu ya
kumuweka fiti viwanja vya Carrington chini ya Mtaalamu wa maungo.
Valencia
na klabu za Uturuki ni miongoni wanaomtaka kipa huyo, wakat United
inamtaka mchezaji huru, Sergio Romero azibe pengo lake.
Mashabiki wa Manchester United walistaajabishwa na jina la Valdes kutokuwemo kwenye kikosi cha Louis van Gaal kilicjokwenda ziara ya kujiandaa na msimu.
"Valdes
hajateuliwa (katika ziara) kwa sababu hafuati falsafa zangu. Falsafa ni
jinsi gani unacheza soka na jinsi gani unalinda ladha ya uchezaji
wako,"amesema Van Gaal.
"Aligoma
msimu uliopita kuchezea timu ya pili. Kuna mengi katika upande mwingine
wa falsafa, namna gani unatakiwa kucheza kama kipa Manchester United.
Kama haujaridhia [kufuata] utaratibu wa falsafa hiyo kuna njia moja tu,
na hiyo ni kuondoka,"amesema Van Gaal.
0 maoni:
Chapisha Maoni