Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » UHURU SULEIMAN APATA ULAJI SOUTH

UHURU SULEIMAN APATA ULAJI SOUTH

IMG-20150716-WA0016[1]

 Mchezaji Uhuru Selemani amesaini mkataba wa miaka miwili na timu ya Jomo Cosmos ya nchini Afrika Kusini. mchezaji huyo ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari nchini humo.

Uhuru selemani anatarajiwa kuvuta kitita cha dola 5000 kama mshahara wake baada ya makato yote ya kodi kufanyika. hii ni hatua kubwa katika maisha ya soka ya Uhuru Selemani na taifa kwa ujumla.
Kabla ya kutimkia Jomo Cosmos Uhuru Selemani alishindwa kufikia muafaka wa kusajliwa na timu yake ya Mwadui F.C ya mkoa wa Shinyanga baada ya kudai dau kubwa ambalo uongozi wa Mwadui uligoma kulipa.
Uhuru Selemani amefanikiwa kuichezea timu ya taifa na pia kabla ya kufika Jomo Cosmos hapa nyumbani alicheza Mtibwa Sugar, Coastal Union, Simba na baadae kuhamia ligi daraja la kwanza na kufanikiwa kuipandisha Mwadui F.C kuja ligi kuu.
IMG-20150716-WA0015[1]
HONGERA UHURU NA KILA LA KHERI
Blog inayotoa habari kila siku Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. JAFAR NZOWA JR - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger