Mashabiki
wa Barcelona wa America kaskazini wame-maindi kinoma baada ya kugundua
kwamba nyota wakubwa wa klabu hiyo hawamo katika ziara ya Marekani
itayoanza wiki ijayo.
Barcelona
wametaja kikosi cha wanandinga 24 wataokwenda ziara ya Marekani
itayoanza Julai 19-29 mwaka huu, lakini nyota wake wawili, Lionel Messi
na Neymar wameachwa kwasababu kocha mkuu, Luis Enrique amewaongezea siku
katika likizo yao.
Messi na Neymar walishiriki michuano ya Copa America iliyomalizika siku za karibuni kwa Chile kuibuka Machampion.
Lakini sio wao tu, wachezaji wote waliocheza Copa America kama vile Claudio Bravo, Javi Mascherano na Dani Alves pia wameondolewa katika ziara hiyo ya Marekani.
HIKI NDICHO KIKOSI CHA BARCELONA CHA WACHEZAJI 24 WANAOKWENDA ZIARA YA MAREKANI
Ter
Stegen, Masip, José Suárez, Piqué, Rakitic, Sergio, Pedro, Iniesta,
Suárez, Rafinha, Bartra, Douglas, Jordi Alba, S. Roberto, Adriano,
Vermaelen, Mathieu, Arda Turan, Aleix Vidal, Sandro, Munir, Halilovic,
Samper, Gumbau
0 maoni:
Chapisha Maoni