Morgan
Schneiderlin, Memphis Depay, Matteo Darmian na Bastian Schweinsteiger
wote wamecheza mechi yao ya kwanza Manchester United ikishinda goli 1-0
dhidi ya Club America katika mechi ya kwanza ya michuano ya International Champions Cup iliyopigwa asubuhi hii uwanja wa Seattle, Marekani.
Schneiderlin ndiye amefunga goli pekee la ushindi dakika 5 tu ya kipindi cha kwanza akimalizia krosi ya Juan Mata.
Mfaransa Depay na Darmian wote walitolewa na Louis van Gaal, huku Schweinsteiger akiingia kucheza mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo.
Schweinsteiger amecheza vizuri na kuifanya United itawale mchezo kipindi cha pili, lakini walishindwa kuongeza bao.
0 maoni:
Chapisha Maoni