Timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagles imempa kibarua cha ukocha kiungo na nahodha wake wa zamani Sunday Oliseh.
Oliseh anachukua nafasi ya Stephen Okechukwu Keshi ambaye alitimuliwa mwanzoni mwa mwezi huu na uongozi wa timu hiyo.
Kocha huyo atasaidiana na mbeligiji Jean Francois Losciuto wakati kikosi hicho kikiwa kinajiandaa kupambana na Tanzania mapema mwezi wa September mwaka huu katika michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika kwa mwaka 2017.
0 maoni:
Chapisha Maoni