Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » KUBENEA, KAFULILA NA MTETEMA WAPEWA TUZO

KUBENEA, KAFULILA NA MTETEMA WAPEWA TUZO

Jaji Mark Bomani (kulia) akimpa tuzo Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers, Saed KubeneaDREAM Success Enterprises, waasisi wa Tuzo ya Shujaa Kati Yetu, wamewatunuku tuzo Saed Kubenea, David Kafulila na Vick Mtetema kwa mchango wa kazi zao zilizotukuka katika maendeleo na ujenzi wa taifa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Kubenea, mwandishi wa habari za uchunguzi, mmiliki wa mtandao wa MwanaHALISI Online na gazeti la MwanaHALISI lililofugwa na serikali kwa muda usiojulikana ametunukiwa tuzo ya “Uwazi na Ukweli.
Wakati Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR – Mageuzi), ametunukiwa tuzo ya “Maono Mapevu” kwa kuibua na kusimamia bungeni ufisadi wa zaidi ya Sh. 300 Bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Naye Mtetema, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Same Sun, linalofanya utetezi wa haki za watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), ametunukiwa tuzo ya “Ubunifu.”
Tuzo hizo zinalenga katika kuleta mapinduzi ya kimaadili na kifikra nchini.
Akizungumza wakati akikabidhi tuzo hizo leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mark Bomani, ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwapa tuzo kubenea, Kafulila na Mtetema kwa kazi nzuri wanazozifanya ni muhimu sana kwa sababu wote ni watu makini.
“Kubenea amejitahidi sana. Gazeti lake ni moja ya magazeti yanayoandika na kusema kweli bila kuogopa, kujipendekeza, kutoonea wala kupendelea. Hicho ndicho kinachohitajika,” amesema Jaji Bomani.
Jaji Bomani amesema japo Kafulila ni Mbunge kijana, lakini ametoa mchango mkubwa katika kutetea rasilimali za taifa kwa kufichua maovu yanayoendelea serikalini. Kazi ambayo inahitaji uelewa, umakini, ujasiri na kusema kweli. Wakati Kamata amejitolea kutetea na kuzungumzia kwa undani suala la mauji ya Albino, hali inayotimia moyo katika mapambano hayo.
Pia, amesema wote ambao wamejitahidi kufikisha ujumbe kwa wananchi lazima wapongezwe na kupewa tuzo kwa jitihada zao. Juhudi kubwa ifanyike kuwasaka wengine mabao wamejitahidi kufichua maouvu ili nchi iwe ya amani.
“Tumezoea kuona watu wakitunukiwa Tunu za Taifa kila mwaka katika sherehe za muungano au uhuru. Hiyo haitoshi. Hizo ni kazi za serikali. Lazima na watu nao wawe na vyombo vyao ambavyo vinawatambua watu ambao wasingetambukika huko serikalini,” amesema Jaji Bomani.
Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Kubenea amesema, “…tuzo hii ni faraja kwangu. Sijutii kuwa mkweli. Gazeti langu la MwanaHALISI limefungiwa na serikali. Karamu yangu inaweza kuvunjwa. Mdomo wangu unaweza kuzibwa. Lakini siwezi kunyamaza.”
Kubenea amefananisha jina la tuzo hiyo la “Uwazi na Ukweli” na kauli ya serikali ya awamu ya tatu ambayo badae iligeuka na kuficha ukweli na kukumbatia usiri. Ikauza mgodi wa Kiwila, nyumba za serikali kwa wasio stahaili na kwa bei ya kutupwa, mashamba ya mkonge, ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania na Benki NBC.
Kwa upande wake Kafulila amesema, “…nimejisikia fahari kubwa kuwa miongoni mwa watu ambao wamechangia chochote katika taifa letu, hata kupewa tuzo hii. Nikifa kesho duniani wanangu, wajukuu, ndugu zangu na watu wengine watanikumbuka kwamba nilifanya chochote.”
“Taifa letu lina tatizo kubwa la watu kukosa uadilifu na kujaa uoga. Hii inatokana na ukosefu wa bidii na maarifa….nachoweza kuwaahidi watu, nitaendelea kuwatumikia. Nakwenda kugombea tena. Nikishidwa, nikishinda sitoacha kutumikia nchi yangu,” amesema Kafulila.
Aidha, Mtetema amesema, “….ni heshima kubwa kutunukiwa hii tuzo. Vitendo vya albino kuuwawa vinakithiri wakati huu wa uchaguzi. Naomba nimteue David Kafulila awe baba na kuwasemea watu wenye albinism bungeni,”
Mtetema amemtaka Kafulila kama atafanikiwa kuchaguliwa katika Bunge la 11 kuhakikisha kunakuwepo na sera ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), Sheria ya kuwaondoa wanganga wanaopiga ramli na mazingira mazuri kwa Albino.
Joshua Lawrence, afisa mikakati toka Dream Success Enterprises amesema maendeleo ya taifa lolote duniani hutengenezwa na raia na viongozi wenye habari, maarifa na maono sahihi. Na ili kufanikisha hayo, uhuru wa kupata habari ndani ya muktadha ni muhimu kuwepo.
“Na, hili linawezekana tu pale raia wanaopewa uhuru wa kuogelea ndani ya bahari ya fikra huru, huku muktadha wa sheria zinazolinda kingo za uhuru huo ukiwa ni kuzinawilisha fikra pevu na kuzinyong’onyeza fikra bwete, wala si vinginevyo,” amesema Lawrence.
Lawrence amesema hiyo ni awamu ya pili tuzo hizo kutolewa. Awamu ya kwanza ilikuwa 22 Disemba, mwaka 2014 ambapo Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh alitunukiwa.
Blog inayotoa habari kila siku Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. JAFAR NZOWA JR - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger