Kiujumla usajili mpya umekuja na matarajio makubwa kwa mara ya kwanza katika klabu tangu kujiuzulu kwa Sir Alex Ferguson, Mei, 2013. Miezi kumi ya David Moyes iliiporomosha timu hiyo hadi katika nafasi ya saba katika ligi kuu msimu wa 2013/14. Licha ya kusaini wachezaji wawili tu ( Marouane Fellaini na Juan Mata), David alifanya kazi na wachezaji washindi.
Vijana kama, Rafael da Silva, Phill Jones, Criss Smalling na wale waliopevuka kama, John Evance, Javier Hernandez, Antonio Valencia, Danny Welbeck, Ashley Young walikuwa sehemu ya timu iliyoshinda taji la mwisho chini, Ferguson miaka miwili iliyopita.
Wote hao walishindwa kupandisha viwango vyao chini ya Moyes, huku wachezaji wazoefu kama, manahodha watatu, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Patrice Evra wakishindwa kuchezeshwa katika mzunguko mzuri kutokana na umri wao mkubwa. Rio, Evra walicheza kwa kiwango cha juu wakati, Ferguson alipokuwa akisaka taji lake la 13 na kombe la 19 upande wa klabu.
Nilikuwa na matumaini makubwa na Moyes kwa kuwa hata Fergie mwenyewe wakati anaondoka alisema alimpendekeza David kuchukua nafasi yake kwa kuwa klabu ili hitaji ' Mtu Hasa wa Manchester'. Moyes alisaidia sana kuhakikisha, Wayne Rooney anaachana na mpango wa kuhamia Chelsea na kusalia United. Lakini wachezaji wakali kama, Michael Carrick, Rooney, Van Persie walishuka viwango vyao. David hakufaa, United kutokana na mbinu zake na kiwango chake kidogo cha ufundishaji wachezaji wakubwa waliozoea kushinda mataji.
VAN GAAL ATAFUKUZWA ENDAPO…..
Van Gaal alitumia zaidi ya pauni 150 milioni katika msimu wake wa kwanza Old Trafford. Angel Di Maria alitua kwa usajili wa rekodi England huku akiwa mshindi wa ligi ya mabingwaia. Luke Shaw, Marcos Rojo na Dael Blind pia walisajiliwa kwa gharama kubwa ili kuziba mapengo ya Rio, Vidic na Evra katika ngome. Andre Herrera na Radamel Falcao wote walianza maisha United msimu uliopita chini ya Mholanzi huyo lakini timu haikutwaa taji lolote.
Target ilikuwa ni kurejea katika michuano ya ulaya kwanza, jambo ambalo lilifanikiwa kwa wastani licha ya wachezaji wa zamani kusema kuwa gharama aliyotumia Van Gaal kuwasaini nyota hao sita alipaswa kugombea taji na si nafasi ya Nne. Kuwaongeza nyota wengine kama Bastian, Matteo, Morgan na Depay inamaanisha kuwa Van Gaal ametengeneza timu mpya kabisa pale Old Trafford huku nahodha Rooney akibaki kama mchezaji asiyegusika kutoka katika timu ya Ferguson.
Matteo anaweza kupangwa kama mlinzi wa kulia katika kikosi cha kwanza, wakati Shaw anaweza kuchukua nafasi ya upande wa kushoto katika ngome. Rojo na Blind wanaweza kuanza sambamba katika beki ya kati mbele ya Smalling na Jones na kama hili litatokea Van Gaal atapigwa vita sana licha ya kuwa katika mikakati ya kutengeneza timu mpya.
Kuwacha nje wachezaji wane wa Kiingereza katika ngome, tena waliosajiliwa kwa gharama kubwa na Fergie inaweza kuwa sababu ya Van Gaal kusakamwa na magwiji wa klabu kama mambo hayatakwenda vile anavyotaka. Hali ya ushindani wa namba itakuwa ni ya kiwango cha juu. Smalling na Jones si wachezaji wa kuwategemea moja kwa moja kwa sababu ni wagojwa na majera ya mara kwa mara.
Fellaini, Bastian na Herrera inaweza kuwa safu ya kiungo ya Van Gaal pale United. Na Huenda timu hiyo ikaingia katika mfumo mpya wa kiuchezaji ili kuendana na klabu nyingine kubwa za ulaya. 4-3-3 inaweza kuwapanga watatu hao katika idara ya kiungo, na kuwaacha Rooney, Mata na Di Maria katika safu ya mashambulizi.
Van Gaal hakika ana kikosi kikubwa ambacho kinaweza kuwatisha wapinzani wake wengi lakini anapaswa kuendelea kuwashikiria wachezaji wa ‘ Mechi za Kiingereza’ kama Young, Valencia, huku akimchagulia mechi muhimu nahodha msaidizi, Carrick. Kushindwa kufika walau robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa kikosi alichonacho ni sawa na k,ushindwa kwani David aliweza kufanya hivyo licha ya kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kuongoza timu katika michuano hiy msimu wa 2013/14.
United itawekeza malengo pia katika michuano ya ndani. Ligi kuu ni kipaumbele cha kwanza wakati, micvhuano ya FA na Capital One ikibaki kama target ya ziada. Msimu uliopita Van Gaal alivumiliwa kwa sababu aliikuta timu ikiwa taabani. Alifungwa na kuondolewa na Arsenal katika robo fainali ya kombe la FA huku akishuhudia timu yake ikiondolewa mapema tena kjwa aibu na timu ya ligi ya chini katika michuano ya Capital. Kumaliza nafasi ya nne katika ligi kuu ilikuwa tarajio la mashabiki lakini magwiji wa klabu hawaridhishwi na hilo tu zaidi ya kuona mataji yakitua klabuni.
Manchester United ni zaidi ya Tangazo la Mpira na Van Gaal anaweza kujikuta akiathiriwa na kelele na nje ya klabu kama ilivyokuwa kwa Moyes. Klabu kubwa ni lazima iwe na mseto wa wachezaji wakubwa tena wenye idadi ya kutosha. Timu mpya ya Van Gaal, kiucherzaji inaweza kuvutia kuliko ile ya Alex Ferguson lakini kimatokeo ni jambo la kusubiri na kuona lakini matumaini ni makubwa kuliko kufeli.
0 maoni:
Chapisha Maoni