Kutoka
katika ukurasa maarufu wa facebook wa 'Naipenda Yanga' kuna taarifa
kuwa, klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji
wa kutegemewa wa Gor Mahia na mfungaji bora wa KPL Michael Olunga
Inaelezwa
kuwa makubaliano ya awali baina ya mchezaji na klabu yamefikiwa huku
Yusuf Manji akisisitiza lazima Mkenya huyo atue Jangwani baada ya
kuvutiwa mno na soka lake.
Ikumbukwe
Olunga aliisumbua mno safu ya Ulinzi ya Yanga na kuweza kufunga goli la
pili katika ushindi wa 2 - 1 walioupata K'ogallo.
0 maoni:
Chapisha Maoni