Takriban
askari wanane wa Afghanistan wamekufa katika shambulio la anga la
Marekani kwenye kituo cha kijeshi cha ukaguzi katika jimbo la Logar
kusini mwa mji mkuu Kabul, kwa mujibu wa maafisa wa Afghanistan.
Wanasema helikopta za Marekani zilishambulia kituo hicho cha ukaguzi wakati wa mchana Jumatatu.Wanajeshi kadhaa wamejeruhiwa.
Kamanda wa jeshi katika eneo hilo ameiambia BBC kuwa kituo hicho cha ukaguzi kilikua kinapeperusha wazi bendera ya Afghanistan.
Hali ya usalama katika jimbo la Logar inayumba ambapo maeneo mengi ya vijijini vimo mikononi mwa wapiganaji wa Taliban.
Mwandishi wa BBC David Loyn aliyeko mjini Kabul anasema kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu tukio la leo asubuhi katika wilaya ya Baraki Barak .
Mwandishi wetu anasema juhudi za uokozi zinatatizwa na makundi ya waasi wanaowashambulia kwa risasi wanajeshi wa Afghanstan.
Msemaji wa vikosi vya kimataifa nchini humo anasema wanafahamu kuhusu tukio hilo linalovihusisha vikosi vya Marekani na kwamba wanalifanyia uchunguzi.
Chanzo: BBC
0 maoni:
Chapisha Maoni