SIMBA VS AZAM
ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YA DIAMOND PLATNUMZ JANA
MAGUFULI NA MAFURIKO CHATO PAMOJA NA WASANII KIBAO
Kundi la Orijino Komedi likikamua jukwaani.
Maelfu wa wakazi wa Chato wakisikiliza kwa makini sera za Mgombea Urais kupitia CCM, John Magufuli.
Wakazi wa Chato wakionesha mabango yao mbalimbali.
Nyomi ya wanachama wa CCM kama inavyoonekana leo hii huko Chato.
Msanii wa Bongo Fleva, Madee akitoa burudani kwa wakazi wa Chato.
Kundi la Yamoto Band wakikamua jukwaani, katikati ni densa wa Yamoto, Chiba.
Staa wa Hip Hop, Fid Q akitoa burudani.
Magufuli akiwafunika Chegge na Temba.
Kundi la Orijino Komedi likikamua jukwaani.
Mgombea Urais kupitia CCM, John Magufuli akiingia Viwanja vya Chato
Mgombea Urais kupitia CCM, John Mafuguli leo alifanya mkutano mkubwa wa kuomba kura katika Viwanja vya Chato ambapo ndipo nyumbani kwake. Mkutano huo ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Katika mkutano huo wasanii mbalimbali walitoa buurudani ambapo walipopanda wasanii wa kundi la TMK Wanaume familiy Chegge na Temba Magufuli alishindwa kujizuia na kuanza kusakata nao jukwaani na kuwafunika wasanii hao hali iliyozua shangwe kubwa kwenye viwanja hivyo.
Sambamba na burudani hiyo Magufuli alimwaga sera na kutoa ufafanuzi wa jinsi atakavyoikwamua Tanzania kutoka katika lindi la umasikini mijini na vijijni.
WANA CCM WAHAMIA ACT
Zaidi ya wanachama 100 kutoka CCM, Kata ya Chihanga, Manispaa ya Dodoma wamejiunga na ACT- Wazalendo.
Akizungumza
kwa niaba ya wanachama hao, Ally Amanzi aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Wazazi wa CCM katika kata hiyo, alisema jana kuwa wamelazimika
kuhama kutokana na kufilisika kisiasa.
Amanzi
alisema viongozi wa vyama hawaonyeshi kama wanaweza kuleta mabadiliko,
badala yake wanafikiria watakavyojilimbikizia mali.
“ACT–Wazalendo
tunaimani nayo sisi wakazi wa Kata ya Chihanga, lazima tutapata
mabadiliko ya kweli tofauti na vyama vingine vinavyojitokeza kuomba
viongozi wao tuwachague,” alisema Amanzi.
Alisema katika chama hicho kuna ubabaishaji mwingi, hali inayochangia wananchi wasipate maendeleo.
Walence
Lusingu ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Mkoa
wa Dodoma, alisema ACT kimedhamiria kuwaletea maendeleo ya kweli
wananchi wa kata hiyo.
Lusingu
ambaye ni mgombea udiwani katika Kata ya Miyuji, aliwataka wakazi wa
kata hiyo kutofanya makosa ya kuchagua viongozi wa vyama vya siasa
ambavyo vitawageuza kuwa mitaji pindi vitakapochaguliwa kushika
madaraka.
Alisema
katika kipindi hiki cha kampeni, lazima wawe makini katika kusikiliza
sera zinazotolewa na wagombea hao, kutokana na wengi wamekuwa wakijinadi
kwa kutoa maneno matamu huku wakiwa siyo wakweli.
Mgombea
udiwani wa Kata ya Chihanga ambaye alikuwa diwani kupitia CCM kabla ya
kuhamia ACT- Wazalendo, Julia Mputu amewaomba wananchi wa kata hiyo,
kumpa ridhaa tena ya kumrudisha madarakani ili amalize miradi iliyobaki
wakati wa kipindi chake.
Mputu
alisema katika kipindi chake cha udiwani, mahitaji ambayo walikuwa
wamemtuma mengi ameyafanikisha na machache hajakamilisha.
Aliyataja baadhi ya mambo aliyofanikisha kuwa ni barabara, afya, elimu pamoja na suala ya kilimo.
Hata hivyo, alisema miradi iliyobaki ataikamilisha watakapomchagua katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.
“Nawaomba
mnirudishe nije tumalizie miradi iliyobaki ukizingatia kuwa kazi yangu
niliyoifanya kwa kushirikiana na ninyi mmeiona kwa vitendo. Hakukuwa na
ubabaishaji wowote,” alisisitiza.
Hiki ndio kikosi cha Simba msimu 2015/2016
Klabu ya Simba imekamilisha usajili ramsi na hiki ndio kikosi chake kitakachoshiriki katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom 2015/2016.
Hii ndio orodha ya wachezaji wote wa Simba waliosajiliwa msimu wa 2015/2016
- Vincent De Paul Angban
- Peter Manyika
- Denis Deonis
- Mohamed Hussein
- Hassan Ramadhani
- Emery Nimubona
- Samih Ali Nuhu
- Hassan Isihaka
- Murushid Juuko
- Mohamed Faki
- Saidi Issa
- Abdi Banda
- Jonas Mkude
- Justice Majabvi
- Awadh Juma
- Saidi Hamisi Ndemla
- Mwinyi Kazimoto
- Peter Mwalyanzi
- Hajibu Ibrahim
- Issa Abdallah
- Daniel Lyanga
- Hamisi Kizza
- Pape Abdoulaye Ndaw
- Mussa Hasan Mgosi
- Boniphace Maganga
- Simon Serunkuma
- Joseph Kimwaga
TIMU ZA VPL NA JEZI ZAO MSIMU HUU
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi, viatu na vifaa vingine vinayohitajika.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.
Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.
Wawakilishi wa kionyesha jezi za Mtibwa Sugar, (picha na michuzi blog) |
“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.
Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
Wawakilishi wa Kagera Sugar wakionyesha jezi za nyumbani na ugenini za timu hiyo (picha na michuzi blog) |
Wakionyesha jezi za Coastal union za nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Mbeya City nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Yanga nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Simba SC za nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
Jezi za Stand United za ugenini na nyumbani |
Picha ya Pamoja katika utoaji wa vifaa vya michezo kwa vilabu |