Zaidi ya wanachama 100 kutoka CCM, Kata ya Chihanga, Manispaa ya Dodoma wamejiunga na ACT- Wazalendo.
Akizungumza
kwa niaba ya wanachama hao, Ally Amanzi aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Wazazi wa CCM katika kata hiyo, alisema jana kuwa wamelazimika
kuhama kutokana na kufilisika kisiasa.
Amanzi
alisema viongozi wa vyama hawaonyeshi kama wanaweza kuleta mabadiliko,
badala yake wanafikiria watakavyojilimbikizia mali.
“ACT–Wazalendo
tunaimani nayo sisi wakazi wa Kata ya Chihanga, lazima tutapata
mabadiliko ya kweli tofauti na vyama vingine vinavyojitokeza kuomba
viongozi wao tuwachague,” alisema Amanzi.
Alisema katika chama hicho kuna ubabaishaji mwingi, hali inayochangia wananchi wasipate maendeleo.
Walence
Lusingu ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Mkoa
wa Dodoma, alisema ACT kimedhamiria kuwaletea maendeleo ya kweli
wananchi wa kata hiyo.
Lusingu
ambaye ni mgombea udiwani katika Kata ya Miyuji, aliwataka wakazi wa
kata hiyo kutofanya makosa ya kuchagua viongozi wa vyama vya siasa
ambavyo vitawageuza kuwa mitaji pindi vitakapochaguliwa kushika
madaraka.
Alisema
katika kipindi hiki cha kampeni, lazima wawe makini katika kusikiliza
sera zinazotolewa na wagombea hao, kutokana na wengi wamekuwa wakijinadi
kwa kutoa maneno matamu huku wakiwa siyo wakweli.
Mgombea
udiwani wa Kata ya Chihanga ambaye alikuwa diwani kupitia CCM kabla ya
kuhamia ACT- Wazalendo, Julia Mputu amewaomba wananchi wa kata hiyo,
kumpa ridhaa tena ya kumrudisha madarakani ili amalize miradi iliyobaki
wakati wa kipindi chake.
Mputu
alisema katika kipindi chake cha udiwani, mahitaji ambayo walikuwa
wamemtuma mengi ameyafanikisha na machache hajakamilisha.
Aliyataja baadhi ya mambo aliyofanikisha kuwa ni barabara, afya, elimu pamoja na suala ya kilimo.
Hata hivyo, alisema miradi iliyobaki ataikamilisha watakapomchagua katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.
“Nawaomba
mnirudishe nije tumalizie miradi iliyobaki ukizingatia kuwa kazi yangu
niliyoifanya kwa kushirikiana na ninyi mmeiona kwa vitendo. Hakukuwa na
ubabaishaji wowote,” alisisitiza.
0 maoni:
Chapisha Maoni