Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Tanzania
bara leo imekabbidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo yenye
thamani ya shilingi milioni 490,00,000.
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es
salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin
Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya
soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi vifaa mbalimbali vy a ligi
ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi, viatu na vifaa vingine
vinayohitajika.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi
siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni
imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa
msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.
Twissa alisema Vodacom inaendelea
kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa
nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao
baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya mchezo waupendao pia siku
zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa
inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato
makubwa ya kodi kutoka sekta hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza
ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji
wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na
wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza
kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi
ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.
|
Wawakilishi wa kionyesha jezi za Mtibwa Sugar, (picha na michuzi blog) |
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya
Ligi, Boniface Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom na kuvitaka vilabu
vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati
wote wa ligi.
“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia
jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama
inavyotakiwa” alisema.
Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia
kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu
izingatie masharti ya madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya
kuwapatia vifaa.
Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora
kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki
zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na
ushindani mkubwa.
|
Wawakilishi wa Kagera Sugar wakionyesha jezi za nyumbani na ugenini za timu hiyo (picha na michuzi blog) |
|
Wakionyesha jezi za Coastal union za nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
|
Jezi za Mbeya City nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
|
Jezi za Yanga nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
|
Jezi za Simba SC za nyumbani na ugenini (picha na michuzi blog) |
|
Jezi za Stand United za ugenini na nyumbani |
|
Picha ya Pamoja katika utoaji wa vifaa vya michezo kwa vilabu |
0 maoni:
Chapisha Maoni