Mgombea ubunge jimbo la Ubungo Saed Kubenea
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) wachapishaji gazeti la MwanaHALISI Saed Kubenea ameahidi kulivalia njuga sakata la Richmond linalodaiwa kuwa ni ajenda ya Dr. Slaa kumchfua mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa.
Aidha, kwa mara pili Dk. Slaa ambaye ni msomi wa thiolojia, amemtuhumu Mgombea Urais anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa kwamba ni fisadi na hafai kuchaguliwa na wananchi huku akimtaja mgombea waCCM Dk.John Magufuli kuwa nidye anayestahili kuwa rais wa Tanzania kwa awamu ya tano.
Kwa mujibu wa Kubenea amesema ameshindwa kuvumilia taarifa anazozitoa Dk. Slaa kuhusu sakata hilo na sasa ataeleza anachokijua kuhusu sakata la Richmond na msukumo uliopo hata Dk. Slaa kujitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi katika mlengo wa kumshambulia na kumchafua Lowassa.
Ameongeza kuwa anatarajia kuongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam kueleza ukweli uliokamilika kuhusu Dk. Slaa na mkewe Josephine Mushumbuzi na sababu ya yeye kususia chama
0 maoni:
Chapisha Maoni