Ripoti hiyo ambayo pia iliorodhesha uhalifu uliotendwa na waasi hapo mwaka jana. Jeshi lilielezewa kufanya mashambulizi ya mambomu kwa njia ya anga na mashambulizi ya ardhini kwa raia pamoja na kuchoma moto vijiji katika kampeni ya kumaliza uasi huko Darfur kaskazini na kusini mwaka 2014.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu ilisema kumekuwepo na ukiukaji mkubwa wa sharia za kimataifa. Walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika-AU na Umoja wa Mataifa-UN ambao wanaunda kikosi cha pamoja huko Darfur wanaojulikana kama UNAMID walielezea kesi 411 za manyanyaso yaliyofanywa na pande zote katika mzozo.
CHANZO: VOA
0 maoni:
Chapisha Maoni