Shikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania leo limesaini mkata mpya wa miaka mitatu na
kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa ajili ya udhamini wa ligi kuu
Tanzania bara ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
Mkurugenzi
wa mawasiliano na masoko wa Vodacom Kelvin Twise amesema, mkataba huo
unaongezeko la asilimia 40 kutoka kwenye udhamini wa miaka iliyopita
ambapo udhamini ulikuwa ni shilingi bilioni 1.6 na mkataba wa sasa
utagharimu shilingi bilioni 2.3.
Twise
amesema ongezeko kubwa la udhamini limekwenda kaktika usafiri wa timu
kwasababu timu nyingi zimekuwa zikilalamika kuwa zinapata wakati mgumu
kwenye gharama za usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwahiyo
katika fedha hiyo ya udhamini, shilingi bilioni 1.2 zitakwenda kwenye
timu zote 16, waamuzi wanagharimu zaidi ya milioni 360, maafisa wengine
wa mechi ambao wanakuwa nje ya uwanja wao gharama yao ni zaidi ya
milioni 62, TFF wao wanapata milioni 183, zawadi kwa ujumla ni milioni
174.
Akaongeza
kuwa hawajaongeza kiasi chochote kwenye zawadi kwasababu waliangalia
kati ya kuongeza zawadi au kuzisaidia timu nyingine mpya na zile zenye
uwezo mdogo kifedha ili ziweze kupambana kwenye ligi, wakaona ni bora
kuongeza kiasi ambacho timu zinapata ili kujiendesha kuliko kuongeza
zawadi. Zaidi ya hapo wataendelea kutoa tuzo ya mchezaji bora wa kila
mwezi kama kawaida ambapo imetengwa milioni 18, mchezji bora wa ligi,
mwamuzi bora, na kocha bora zenyewe zimebaki kama zamani.
Kwa maana hiyo, ongezeko limekwenda sehemu tatu, kwanza kwenye timu, waamuzi na match officials.
Rais
wa TFF Bw. Jamal Malinzi akafafanua kuhusu mkataba huo jinsi
unavyoiruhusu TFF kutafuta wadhamini wengine wa ziada kwenye ligi kuu
ambayo inadhaminiwa na Vodacom ilimradi yasiwe makampuni yanayoshindana
na mdamini mkuu wa sasa (Vodacom) katika biashara na akaongeza kuwa,
mpaka sasa kwa kushirikiana na Vodacom tayari wameshaanza kutafuta
makampuni mengine.
Katika
hatua nyingine, Malinzi amesema TFF inapambana na rushwa kwasababu
inachangia kwa kiasi kikubwa kushusha soka la Tanzania ambapo
iliifananisha rushwa na‘ngono’ kutokana na kufanyika kwa usiri mkubwa
lakini akawaomba wadau wa soka wasaidiane na TFF ili kuweza kuwabaini
watoaji na wapokeaji rushwa wanaoliharibu soka la Tanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni