Mchezaji aliyeingia kutokea benchi
Pedro Rodriguez aliifingua timu yake bao la ushindi katika dakika za
nyongeza ambapo Barcelona walishinda kombe la Eefa Super Cup mchezo
uliopigwa kwenye mji wa Tbilisi.
Washindi wa kombe la Europa
Sevilla waliwashangaza Bacelona ambao ni washindi wa klabu bingwa barani
ulaya baada ya Ever Banega kufunga goli la kwanza kwa mkwaju safi wa
adhabu ndogo.Lionel Messi alifunga mara mbili na kuifanya Barca kuongoza kwa goli 2-1 kabla ya Rafinha na Luis Suarez kufumania nyavu na hivyo matokeo kuwa 4-1. Mabao ya Jose Antonio Reyes,Kevin Gameiro na Yevhen Konoplyanka yaliufanya mchezo huo kwenda dakika 30 za nyongeza kabla ya Pedro kuifungia Barca goli la ushindi.
Haya ni mafanikio makubwa kwa Barcelona tokea mwaka 2011 baada ya kushinda mataji matano mfululizo na kuwa sawa na klabu ya AC Milan ya Italia yenye rekodi sawa na hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni