Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi imeyataka majimbo matano nchini Tanzania kurudia mchakato wa kura za maoni ambao ulimalizika wiki iliyopita huku baadhi ya maeneo matokeo yakipingwa vikali.
Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao wa Hivisasa nje ya makao makuu ya CCM mkoani Dodoma katibu wa Itiakadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kutokana na kasoro zilizojitokeza kamati kuu imeagiza majimbo matano yarudie kura za maoni na zoezi hilo lifanyike kesho kutwa siku ya alhamisi tarehe 13,8,2015 na matokeo yake yataletwa kwa ajili ya uamuzi.
Nape ameyataja majimbo hayo kuwa ni Rufiji, Kilolo, Makete, Busega na Ukonga.
Matokeo katika baadhi ya majimbo hayo ni,
JIMBO LA MAKETE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binillith Mahenge, ametetea nafasi yake katika jimbo la Makete baada ya kuibuka mshindi mwembamba.
JIMBO LA UKONGA
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa amepata ushindi wa kura 10,000 dhidi ya Raesh Patel kura 7,356 na Rober Masegesi kura 548.
“Majimbo hayo matano yatarudia uchaguzi wa kura za maoni kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo” Amesema Nape
Katika Hatua nyingine Nape amesema vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vina endelea katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
0 maoni:
Chapisha Maoni