Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Wilbroad Slaa akiwa na mke wake Josephine Mushumbusi
Mke wa Dk. Slaa, Josephine Mushumbusi, amekanusha tuhuma zilizozagaa
kuwa yeye ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema, kujiuzulu na
kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama jambo ambalo amedai kuwa halina
ukweli wowote.
Akijitetea amenukuliwa akisema kuwa “Mwenyewe najiuliza nini
kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba yangu ina milango
miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata watoto siwezi
kuwafungia,”.
Amedai kuwa kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya kwa mwanamume na kuongeza kuwa mwanaume ni mwanaume tu.
0 maoni:
Chapisha Maoni