Mashabiki wanne wa kilabu ya Chelsea
walioshtumiwa kwa kukataa kumruhusu mtu mmoja mweusi kuingia katika treni
ya Paris Metro mashabiki hao wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi za soka kwa
takriban miaka mitano.
Richard Barklie,kutoka Carrickfergus,Northern Ireland na Joshua Parsons pamoja na William Simpson wote kutoka Surrey walipigwa marufuku kwa miaka mitano katika mahakama ya Stratford.
Jordan Munday ,kutoka eneo la Sidcup Kent,alipigwa marufuku ya miaka mitatu.
Waliagizwa kwamba hawawezi kuhudhuria mechi nyumbani ama ugenini.
Jaji wa wilaya Gareth Branston alisema kwamba chuki ya kibaguzi zilionyeshwa na mashabiki wa Chelsea katika treni hiyo ya Paris.
Aliaambia mahakama hiyo kwamba kisa hicho kiliharibu sifa ya soka ya Uingereza barani Ulaya.
Ghasia zilizuka wakati mashabiki wa Chelsea walipokuwa katika mji huo wa Ufaransa ili kushabikia mechi ya vilabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Pasris Saint Germain tarehe 17 februari.
Baadaye kanda ya video iliibuka ikimuonyesha raia mmoja wa Ufaransa Souleymane Sylla akisukumwa nje ya treni.
0 maoni:
Chapisha Maoni