Kocha wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm amekosoa kadi aliyopewa Mchezaji wake Donald Ngoma na kusema ni wazi kwamba kwa mchezaji profesheno kama Ngoma hakusatahili kufanya makosa kama yale lakini kwa kuwa imeshatokea hana la kufanya.
“Kilichotokea hakikuwa sawa kulingana na maamuzi aliyoyachukua Ngoma, yeye kama mchezaji profesheno alipaswa kutambua kwamba tayari ana makosa na ana kadi moja hivyo ilimpasa kujilinda lakini akalisahau hilo na mwisho yakatokea yaliyotokea,” alisema Pluijm.
Kocha wa Simba, Mwingereza, Dylan Kerr, aliyekuwepo uwanjani hapo, naye alizungumza juu ya hilo: “Alichokifanya si kitendo cha kiuchezaji, amekuwa na hasira akashindwa kujizuia na akaigharimu timu na hasara ni kwa Yanga sasa, mchezaji hutakiwi kuwa hivyo halafu ukizingatia ni mtu muhimu, anapaswa kufuata falsafa za michezo uwanjani na kuisaidia timu yake na si vingine.”
Ngoma atakuwa nje ya uwanja kwenye mechi inayofuata dhidi ya Telecom ya Djibouti itakayopigwa keshokutwa Jumatano, kisha kurejea kwenye mechi dhidi ya KMKM ya Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni