Baada ya Boyfriend wa Nicki Minaj, Mr. Meek Mill kumshushia maneno ya kejeli rapa mwenzake Drake kwa kumwambia kwamba hajui kuandika mashairi, sasa Nicki Minaj naye amefunguka yake yaliyomkwaza kwa kutumia akaunti yake ya twita.
Minaj, amewauliza swali waandaji wa tuzo za MTV kwa upande wa nchi ya Marekani , ni kwa nini hawajaitaja vide yake alioishirikiana na Beyonce “ Feeling Myself “ kuingia kwenye kipengele cha video bora ya mwaka ?.
Licha ya kushukuru kutajwa kwake kwenye vipengele vitatu ambavyo ni Best Female Video, Best Hip Hop Video “Anaconda”, na Best Collaboration “Jessie J, Ariana Grande, Nicki Minaj – “Bang Bang” “ , lakini Nicki Minaj bado alihoji uwepo au kutajwa kwa video ya Feeling Myself.
Nick Minaj aliandika “Hey guys @MTV thank you for my nominations. Did Feeling Myself miss the deadline or…? akimaanisha kwamba je video ya Feeling Myself ilichelewa kutoka au ?.
Tuzo hizo za MTV, za huko Marekani zinatarajiwa kutolewa siku ya jumapili ya augost 30 katika jiji la Los Angeles huku Miley Cyrus, akitarajiwa kuwa host wa onyesho jilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni