Mlinzi wa kushoto wa Chelsea Filipe
Luis anakaribia kuihama klabu hiyo baada ya kuichezea kwa mwaka mmoja,
hii ni kwa mujibu wa kocha mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho.
Mchezaji
huyo raia wa Brazil amechezea mara 26 tangu aliposajiliwa na Chelsea
akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha paundi milioni 15.8 wakati wa
msimu wa joto. Hata vilabu hivyo viwili vimekubaliana mchezaji huyo
arejee kwenye klabu yake ya zamani.Mourinho amesema" Kwa wakati huu tunahitaji beki wa kushoto kwa sababu nafikiri tutamuuza Fillipe Luis leo au kesho.
Chelsea inadaiwa kuwa ina mpango wa kumnunua beki wa kushoto kutoka Augsburg, Abdul Baba Rahman.
0 maoni:
Chapisha Maoni