Jeshi
la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam inawashikilia watu wawili
akiwemo mtoto wa miaka 15 kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya
ujambazi likiwemo tukio la uvamizi na mauaji kituo cha Polisi
Stakishari.
Mbali
na hilo jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki 16 kati ya hizo 14
ziliibiwa katika tukio la stakishari, ambazo zilikuwa chini ya handaki
Wilaya ya Mkuranga pamoja na milioni 170.
Suleiman Kova alisema
watuhumiwa hao pamoja vitu hivyo vilikamatwa kutokana na msako wa
unaoendelea wa kupambana na makosa mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia
silaha za moto.
“Julai
17 zilipatikana taarifa za eneo la Taungoma kulikua na majambazi
waliohusika kwenye tukio la stakishari, wakijiandaa kufanya tikio la
uhalifu, kikosi kilikwenda haraka eneo la tukio na kuweka mtego na
kufanikiwa kuwanasa washukiwa watano…walainza kupambana baada ya
kukataa kusimama na majambazi watatu walifariki dunia”Kova.
Alisema
silaha 14 zilizopatikana ziliporwa katika kituo cha stakishari bado
hazijakamilisha idadi ya zilizopotea na jeshi hilo bado linaendelea na
msako.
Kova alisema ndani ya shimo pia wlaikuta silaha ya kichina aina ya Norinko ambayo
haitumiwi na majeshi ya Tanzania, risasi 25 pamoja na fedha taslimu
milioni 170 ambazo zilifungwa katika sanduku maalum la kabati.
0 maoni:
Chapisha Maoni