Yule
komediani mtukutu wa Uingereza, leo ametoa mpya baada ya kuvamia mkutano wa
waandishi wa habari aliokuwa akiendesha Rais wa Fifa, Sepp Bllater aliyetangaza
kujiuzulu na kumwaga noti feki za dola.
Simon
Brodkin ambaye vipindi vyake vimekuwa vikimhusisha mwanasoka Jason Bent na Lee
Nelson, alivamia mkutano huo, wengi wakiamini ni mmoja wa waandishi na kuanza
kumwaga dola hizo za bandia.
Aliendelea
kumwaga fedha hizo kwa Blatter kama sehemu ya rushwa huku akisema: “Hizi ni kwa
ajili ya Korea 2026.”
Alikuwa
akimaanisha anamhonga Blatter ili aipe Korea uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka
206.
Hali hiyo
ilimfanya Blatter abaki amepigwa butwaa kabla ya walinzi kuingia na kumtoa
Brodkin.
Kawaida
Brodkin amekuwa akifanya hivyo sehemu mbalimbali. Hivi karibuni alimvamia
jukwaani Kanye West wakati akitumbuiza na yeye kuanza kutumbuiza.
Kabla
ya hapo, aliwahi kutoa kali alipoungana na wachezaji wa timu ya taifa ya
England akizuga naye ni mchezaji lakini akashitukiwa hatua ya mwisho wakati
akikaribia kupanda ndege.
ALIPOZUGA NI MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND...
0 maoni:
Chapisha Maoni