Mchora katuni mashuhuri Masoud Ally Kipanya alimaarufu kama Kipanya amefunguka na kusema kuwa amekuwa akishawishiwa na watu wengi sana kuingia katika siasa na kufanya siasa kutokana na harakati zake za kuikosoa Serikali na viongozi kupitia sanaa yake ya uchoraji, Masoud alisema hayo alipokuwa akichat Live Kikaangoni Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV.
Moja ya shabiki alitaka kujua kama Mchoraji huyo anaweza kuingia katika siasa na kugombea nafasi ya Ubunge ili aweze kuwakilisha wananchi bungeni na kuweza kufikisha mawazo yake ambayo huwa anayafanya katika kurekebisha au kukumbusha Serikali pamoja na viongozi mbalimbali kupitia sanaa yake ya uchoraji wa katuni.
“Kwa sasa sijajua bado ,ingawa nashawishiwa na watu lakini bado naiogopa siasa, sijaamu ingawa bado ila naamini naweza kuwasaidia watanzania bila ya kuwa mbunge, diwani au rais. kupitia hizi hizi fani zetu za sanaa “
Mbali na hilo Masoud Kipanya alisema kupitia sanaa yake ya uchoraji ni moja ya kitu ambacho kwa sasa kinamuingizia pesa nyingi kuliko kitu kingine chochote akifanyacho na kudai kuwa sanaa hiyo hiyo imeweza kumpa nafasi ya kufahamiana na watu na pia imempa nafasi ya kuifahamu dunia, ingawa anakiri wazi kupitia kazi yake hiyo ya uchoraji muda mwingine huwa anapata vitisho kutoka kwa viongozi ambao wanakuwa wamechorwa na kutafsiri tofauti kile alichokichora na kudai kuwa changamoto hiyo inakwenda mpaka kwa wahariri kwani kuna muda wanaogopa kuchapisha baadhi ya katuni zake.
“Sanaa imenipeleka sehemu kubwa sana ya dunia. imenipa heshima kubwa sana, lakini pia inanilipa sana. pato langu kubwa linatoka kwenye uchoraji sema napata changamoto na kubwa ni pale wanaochorwa wanapokasirika na wakati mwingine kusababisha matatizo hata ya vitisho. lakini changamoto nyingine ni wahariri wa magazeti ninayofanyia kazi kuziogopa baadhi ya katuni na kutozichapisha”
“vitisho viko vingi sana. sana kabisa, bahati nzuri wanasiasa wengi wameingia katika siasa wamenikuta ninachora katuni, hiyo imesaidia sana kuwafanya wengi wao waniheshimu na wakati mwingine hata kuogopa.” Aliongeza Masoud Kipanya.
Mchora katuni maarufu bwana MASOUD KIPANYA.
MAISHA PLUS
Maisha ni kipindi cha Televisheni ambacho huwa kinafanyika mwaka lakini kwa mwaka huu Masoud Kipanya ameonyesha wasiwasi kwa kipindi hicho huenda kisiweze kufanyika kutokana na upungufu wa pesa kwa ajili ya kuendesha kipindi hicho lakini pia aliweza kuweka wazi faidi kubwa yeye aipatayo katika kuendesha kipindi hicho ni kuona analeta mabadiliko ya kujitambua kwa vijana.
“Maisha Plus inafanyika kila mwaka lakini mwaka huu tunaweza tusiifanye kutokana na changamoto za kifedha, maisha plus huwa inagharimu pesa nyingi sana na moja ya faida ya kwanza kubwa na muhimu kwangu mimi katika kipindi cha Maisha Plus ni kuona nasaidia kuleta mabadiliko ya kujitambua kwa vijana.”
Hivyo naweza kusema Maisha plus ipo, mwaka huu tunaweza tusiifanye ingawa bado tuko kwenye mazungumzo na wadhamini wetu ambao tumefanya nao kwa miaka miwili mfululizo, wanataka tupunguze bajeti na sisi tunaogopa kupunguza kwa sababu gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa sana”
Lakini mbali na hilo Masoud Kipanya aliweza kuelezea kwanini imekuwa ni ngumu sanaa kwa baadhi ya washiriki na washindi wa matamasha mbalimbali ya kuonyesha vipaji na kusema kuwa imekuwa ni ngumu sana kwa waandaaji wa matamasha hayo kuwafuatilia washiriki na washindi baada ya muda wao kupita na kusema kuwa muda mwingine familia zinakuwa zinawawekea ukuta waandaaji hao kwa kuhisi kwamba watatumia hizo pesa wanazokuwa wameshinda watu hao jambo ambalo linafanya watu washindwe kuwafanyia mipango watu hao maana wanakuwa mbali nao.
” Kwa hapa nyumbani hatuna mfumo mzuri wa ufuatiliaji hasa baada ya mashindano kumalizika, nikiwa kama muaandaaji, hiyo ni changamoto kwetu. lakini pia mara nyingi mtu akishinda, famili huwa haipendi aingiliwe katika mipango yake wakiamini pengine mtaitolea macho zawadi aliyopata jambo ambalo linaleta umbali mkubwa kati ya muaandaaji na mshindi”
0 maoni:
Chapisha Maoni