Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » YANGA YAONDOKA DAR

YANGA YAONDOKA DAR

Msafara wa Mabingwa wa kandanda nchini Tanzania, Dar es salaamYoung Africans ukiwa na viongozi,wachezaji na  benchi la ufundi umeondoka leo saa 12 alfajiri kuelekea Mbeya.

Yanga itapitiliza moja kwa moja  mpaka Mbozi ambako siku ya jumapili (kesho) itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kimondo FC na mapato yote ya mchezo huo yatachukuliwa na Kimondo FC.


Baada ya mchezo huo timu itaelekea Tukuyu kwa ajili ya kambi,itarudi Mbeya Mjini katika dimba la Sokoine zaidi ya mara 2 kukabiliana na Zesco ya Zambia pamoja na Big Bullets ya Malawi,bila kuusahau mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbeya City.

Haya yote ni maandalizi ya ligi kuu bara msimu 2015-2016 na dhidi ya Azam FC katika mtanange wa Ngao ya Jamii.
Blog inayotoa habari kila siku Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. JAFAR NZOWA JR - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger