|
Muda
mfupi uliopita nimepita katika viwanja vya buguruni sheli ambapo leo
chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE (ADC) wamefanya mkutano mkubwa
wa hadhara wenye lengo la kuwatambulisha wagombea wao wa nafasi za
Urais wa Tanzania na ule wa zanzibar kwa wananchi ambapo mkutano huo
umehudhuriwa na mamia ya wanachama na wakazi wa maeneo ya karibu na
viwanja hivyo.
Pichani katikati ni mgombea wa nafasi ya Urais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania CHIEF LIEMBA akiwa amemshika mkono
mgombea wa nafasi ya Urais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar HAMAD
RASHID kulia kwake,huku kushoto akiwa ni mgombea mwenza wa urais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania SAID MIRAJ wakati wakijitambulisha kwa
mara ya kwanza kwa wananchi tangu wateuliwe na mkutano mkuu kupeperusha
bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hapa nimekupa uhondo wa picha zaidi ya 20 za mkutano huo uliomalizika muda mfupi uliopita hapa Buguruni Jijini Dar es salaam |
0 maoni:
Chapisha Maoni