‘Muvi yetu inaendelea’ pengine hili linaweza kuwa jibu la ‘Actress’ Wema Sepetu, kwa wale wote wanaomshambulia vikali mtandaoni baada yay eye kujikita kwenye siasa.
Madame yupo mjini Dodoma ambapo vikao vya uteuzi wa wagombea CCM, vinaendelea vikiongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete, kupitia ukurasa wake Instagram unaokaribia kuwa na ‘Followers’ laki 9 ‘Bishost’ huyo aliweka picha akiwa na Rais pamoja na muigizaji mwenzie Steve Nyerere kama inavyoonekana hapo juu.
‘Caption’ ndiyo ambayo imeleta utata ikitafsiriwa kwamba ni kama dongo kwa Haters wake, huku kauli mbiu yake ya ‘wamoja havai mbili’ ikiendelea kama kawaida.
“Wakati nyie mnaongea upuuzi… Yangu yaninyookea….. Alhamdulillah… Wa moja havai mbili… Abadan asilan…. Earlier today… Ikulu… Dodoma… Thank u Mr.President” ameandika Wema.
0 maoni:
Chapisha Maoni