Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » MISS TANZANIA USA AVAA TAJI KWA DK 45 NA KUVULIWA

MISS TANZANIA USA AVAA TAJI KWA DK 45 NA KUVULIWA

Aeesha Kamara sasa ndiye mshindi wa Miss Tanzania USA pageant
Aeesha Kamara sasa ndiye mshindi wa Miss Tanzania USA pageant

Doreen Panga kutoka New York usiku wa Aug 22, 2015, alivuliwa taji la Miss Tanzania USA na majaji wa shindano hilo nje ya ukumbi taji alilolivaa kwa dakika 45 na kumvika Aeesha Kamara wa Maryland kwa madai kwamba Doreen Panga hakua chaguo lao.
Majaji hao Peter Walden, Elaine Roecklein, Tee Thompson, Bertini Huemegni,Tina Semiti Magembe, Mayor Mlima, Uche Ibezzue wakiongozwa na Michael Lewis McBride kwa pamoja walikataa kukubaliana na mshindi aliyetangazwa na kufanya kikao nje ya ukumbi wakati watu wakiondoka ondoka nao wakisikitishwa na maamuzi ya kutangazwa mshindi .

 Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Doreen Panga baada ya kuvikwa taji la Miss Tanzania USA
Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Doreen Panga baada
ya kuvikwa taji la Miss Tanzania USA
huku na kama majaji wangekaa kimya basi masahabiki wa shindano hilo wangepelekea lawama kwa
majaji.Jaji Dr. Secelela Malecela japo kwamba alipingana na Doreen Panga kutangazwa mshindi lakini hakukubaliana na majaji wenzake Doreen avuliwe taji na apewe Aeesha Kamara aliyekua chagua la majaji wengine, yeye alipendekeza kwa kua kosa lishafanyika waachane nalo wahakikishe mwakanihalitokei tena, Wazo lake lilipingwa na majaji wenzake pale pale.
Shindano hilo lilianza vizuri kwa nyimbo za Taifa za Marekani na Tanzania zilizoongozwa na watoto Brian akiwa kwenye kinanda na dada yake Briana akiwa kwenye kipza sauti, Baadae walitambulishwa ma miss wa kesho watoto wa DMV wenye umri wa miaka 9 na 12 na baada ya hapo waliingia malikia wenyewe huku wakisindikizwa na wimbo wa Diamond wa mdogo mdogo na
baadae kujitambulisha kwa majaji.

Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Aeesha Kamara baada kuvikwa taji na maamuzi ya majaji ambao hawakukubaliana na mshindi aliyetangazwa kwanza.
Miss Africa 2014-15 akipata picha ya
pamoja na Aeesha Kamara baada kuvikwa taji na maamuzi ya majaji ambao
hawakukubaliana na mshindi aliyetangazwa kwanza
.

Washiriki wa miss Tanzania USA walikua Rechel Mujaya kutoka Atlanta, Joyce Mkapa toka New York, Doreen Panga toka New York, Aeesha Kamara toka Maryland, Aziza Gama toka Maryland
na Brenda Panga toka New York. Washiriki walianza shindano kwa kujielezea wakifuatia na shindano la vipaji na baadae kujibu maswali ya majaji.
Sasa Miss Tanzania USA ni Aeesha Kamara.
Blog inayotoa habari kila siku Karibu Ungana na Mwandishi wetu kila siku hapa Jafar Nzowa

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. JAFAR NZOWA JR - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger