Aidha kikao hicho kitajadili hatua hiyo na kufanya maamuzi juu ya hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki hadi hapo Chama kitakapomchagua mwanachama mwengine kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti.
Kwa mujibu wa taarifa iiyotolewa na ismail jussa ambaye ni kaimu mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano na umma amesema kwamba Katika kipindi hiki, Chama kinawataka wanachama na wapenzi wake wote kuwa watulivu na wavumilivu na kusubiri maelekezo ya vikao vya juu vya kitaifa vya Chama.
Akizungumzia kujiuzulu kwa Prof.Lipumba Jusa amesema Chama hicho kimezipokea taarifa hizo na kinayaheshimu maamuzi yake pia ni haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona yana maslahi kwake.
Katika hatua nyingine amewahakikishia wanachama kuwa CUF itaendelea na shughuli zake kama Chama na pia kama mshirika katika UKAWA ambayo CUF ilikuwa ni katika waasisi wake.
“Tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itatumia nguvu, uwezo, juhudi na maarifa yake yote kuhakikisha kwamba inaulinda UKAWA ambao unaonekana kuwa mwiba kwa CCM.”Amesema Jussa
0 maoni:
Chapisha Maoni