Baadhi ya kauli kutoka kwenye vinywa vya wanasoka mbalimbali juu ya winga na mshambuliaji hatari kwa sasa duniani Cristiano Ronaldo.
Jose Mourinho "Ronaldo ni bora. Ni bora duniani, ndio. Pia ni bora kabisa. Nilimuona Maradona mara kibao. Sikuwahi kumuona Pele, lakini Cristiano anashangaza. Huyu kijana ni bora.... Cristiano ni mashine ya magoli. Yupo kama Zidane, hawezi tokea Ronaldo mwingine"
Alex Ferguson "Baada ya kucheza na Sporting wiki iliyopita, Kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vijana wangu walikuwa wanamzungumzia sana, lakini tukiwa kwenye ndege wakati tunarudi tulishauriana kumsajili, hapo ndipo walipotupangia bei yake"
Henrik Larsson "Ana uwezo wa kufanya mchezo mgumu kuwa mwepesi"
Pele "Ronaldo ametokea kuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa miaka kadhaa, nadhani kwa sasa hakuna shaka Ronaldo ni bora"
Ryn Giggs "Pindi Cristiano Ronaldo akipata mpira, unaweza kuuacha mpira kwake huku akimpiga chenga mmoja baada ya mwingine"
Luis Figo "Ronaldo anaweza kufanya chochote kama mchezaji. Kuna vitu anavifanya akiwa na mpira na kunifanya nishike kichwa kushangaa anachokifanya"
Toni Kroos "Kwa sasa hakuna mchezaji bora zaidi ya Cristiano. Ni miongoni mwa waliokuwa wananifanya nionekane, ni kijana mzuri"
Fernando Torres "Kwa upande wangu yeye ni bora kabisa duniani, ni mashine ya kufunga ambayo huwezi kuifananisha"
Hizo ni baadhi ya kauli zilizo tolewa kumuhusu Cristiano, mchezaji ambaye ameonekana kuwa na mafanikio kila anapokwenda.
0 maoni:
Chapisha Maoni