Mshambuliaji kutoka nchini Chile, Arturo Vidal ameomba kuondoka kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus ili aweze kupata mahala pengine pa kusaka mkate wake wa kila siku.
Mtendaji mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta, amethibitisha kupokea ombi la mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, huku akisistiza huenda mchakato wa kuondoka kwake ukakamilishwa siku za karibuni.
Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wanatajwa kuwa katika mawindo ya kumsajili Vidal na tayari ada ya usajili wake imeshatangazwa kuwa ni paund million 25.9.
Vidal pia anadaiwa kukubaliana na viongozi wa klabu hiyo ya mjini Munich, mshahara wa paund elfu 90 kwa juma.
Vidal anakuwa mchezaji watatu kuondoka Juventus katika kipindi hiki, baada ya kushuhudia Carlos Tevez pamoja na Andrea Pirlo wakifunguliwa mlango kutokea huko mjini Turin.
Kikosi cha Juventus ambacho kipo chini ya meneja Massimiliano Allegri, kimekua kikiongezewa nguvu kwa baadhi ya wachezaji kusajili katika kipindi hiki ambao ni Mario Mandzukic, Sami Khedira pamoja na Paulo Dybala.
0 maoni:
Chapisha Maoni